Virusi vya corona:Elimu kuhusu virusi vya COVID-19

Mlipuko wa maambukizi ya corona umeathiri mataifa mbalimbali duniani, na watu wakiwa wanajiuliza swali kuu moja: Maambukizi ya ugonjwa huu yakoje?

Ninawezaje kujilinda na namna gani virusi hivi vinasambaa?

Maswali kadhaa yamekuwa yakiulizwa na wananchi kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Je, barakoa(mask)inasaidia kukinga maambukizi ya virusi vya corona

Kuna ushahidi mdogo sana kuwa barakoa inasaidia kwa namna moja au nyingine.

Wataalamu wanasema kuwa usafi wa mara kwa mara wa watu kuosha mikono na kutojigusa mdomoni kunasaidia zaidi.

Je, virusi vya corona vinaweza kupatikana katika vitasa vya milango na vinaweza kukaa kwa muda gani?

Kama mtu ana maambukizi na akikohoa katika mkono wake na baadae kushika kitu , je kitu hicho kinaweza kupata maambukizi.

Vitasa vya mlango ni mfano mzuri zaidi kuwa kuna hatari kubwa ya kupata maambukizi kama mtu mwenye corona akishika mlango wakati alikoholea mkono wake.

Wataalamu wanadhani kuwa virusi vya corona vinaweza kukaa kwa muda wa siku kadhaa.

Hivyo namna nzuri ya kukabiliana na jambo hili ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi ni kunawa mikono mara kwa mara.

Je, nikikutana kingono naweza kupata maambukizi?

Haijawa wazi kama watu wakikutana kimwili wanakuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya corona.

Kwa sasa ni kukohoa na kupiga chapya ndio mambo yanayotajwa kuwa hatari katika maambukizi.

Kuna utofauti gani kati ya corona na mafua?

Dalili za maambukizi ya virusi vya corona na mafua yanafanana kwa kiasi kikubwa, hivyo inafanya tiba kuwa ngumu bila kupimwa .

Dalili za virusi vya corona vinaweza kuanza kwa homa na kukohoa.

Mafua mara nyingi huwa yana dalili nyingine kama koo kuwasha, huku watu wenye virusi vya corona huwa wanaweza kuishiwa pumzi kidogo.

TOFAUTI KATI YA CORONA NA MAFUA

Je, virusi vya corona vinaambukiza zaidi ya mafua?

Ni mapema mno kuweza kulinganisha lakini virusi vyote vinaambukiza.

Kwa wastani virusi vya corona vinaweza kuambukiza watu wawili au watatu huku virusi vya mafua huwa ni kama vinatoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine.

Ingawa maambukizi yote ya mafua na corona huwa yanasambaa kwa haraka.

Je,mtu anaweza kupata virusi vya corona kwa kula chakula kilichoandalia na mtu mwenye maambukizi ya corona? –

Mtu mwenye maambukizi ya corona kama amepika bila kuzingatia usafi basi moja kwa moja anaweza kumuambukiza mtu mwingine virusi vya corona.

Virusi vya corona vinaweza kusambaa kwa matone ya kikohozi yaliyo kwenye mkono.

Kuosha mikono kabla ya kushika na kula chakula ndio ushauri unaotakiwa kuuzingatia.

Nichukue tahadhari gani?

Kwa watu wanaoishi Italia na maelfu ambao wanasafiri maeneo mbalimbali duniani, wako kwenye hatari ya maambukizi zaidi.

Maambukizi yanasambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, kwa njia ya matone ya kikohozi.

Ni muhimu kwa watu kuzingatia kuosha mikono mara kwa mara kwa maji yanayotiririka na sabuni au dawa ya kuosha mikono(sanitiser).

Ni vyema kujizuia kuwa karibu na mtu anayekohoa au mwenye homa.

Mtu yeyote anayedhani kuwa amepata maambukizi ya corona ni bora kupigia simu daktari.

Hatua za Kujikinga na Virusi Vya CORONA

Inawezekana ugonjwa huu kupata chanjo?

Kwa sasa hakuna chanjo ya kujikinga na virusi vya corona, ingawa wanasayansi bado wanapambana kutengeneza chanjo ya aina hiyo.

Hivi ni virusi vipya ambavyo havijawahi kumpata binadamu kabla.

Je, mabadiliko ya tabia nchi yanachangia athari zinazojitokea katika virusi vya corona?

Haijawekwa wazi kama mabadiliko ya hali ya hewa yanachangia maambukizi.

Baadhi ya virusi kama vya mafua huwa vinakuja mara nyingi katika wakati wa baridi kali.

Je, mtu aliyeugua ugonjwa wa corona anaweza kupata maambukizi tena?

Virusi hivi vipya vya corona , vinaweza kukusababisha mtu uugue na wengi ni watu wenye shida ya mapafu.

Lakini virusi hivi vipya hakuna ambaye ana kinga dhidi yake.

Hivyo haijalishi kama uliugua mwanzo au la.

Aidha shirika la afya duniani limesema kuwa kabla ya miezi 18 kupita chanjo ya corona itakuwa imepatikana.

CHANZO:BBC.COM